Uzuri Wa Dari Za Jasi Kenya – Gypsum Ceilings

Dari za Jipsam Kenya - Jasi

Je! unahitaji dari za kuvutia na pia mawaidha kutoka kwa watalaamu wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi wa dari hapa Kenya? Gypsum Ceiling Supplies ni kampuni ambayo inaunda na kuuza ceilings (Dari) tofauti za nyumbani na majumba ya biashara nchini Kenya.

Miongoni Mwa Nyenzo za Dari Tunazohusiana Nazo

 • Dari za jasi (Gypsum Ceiling)
 • Dari za akustiki (Acoustic Ceilings)
 • Dari za plastiki (Acoustic Ceilings)
 • Dari za mbao ya kushikamana (TNG Ceilings)
 • Dari za chipboard (Chipboard Ceilings)

Sisi ni Wauzaji Wakuu Wa Dari za Gypsum Kenya

Gharama ya dari ya jasi nchini Kenya ni kati ya Shilingi 2,000 hadi 3,500 kwa kila Mita ya mraba kulingana na kila muundo maalum kutoka rahisi hadi ngumu. Gypsum Ceiling Supplies inatoa huduma za kitaalamu za usakinishaji popote nchini Kenya. Timu yetu ya kubuni na kusakinisha inapata mafunzo ya kina – ndani na nje ya nchi ili kujifunza na kuboresha mitindo ya kisasa ya upambaji wa mambo ya ndani. Urembo na uimara ndio kipaumbele chetu cha kwanza. Tumebobea katika uwekaji wa kazi za jasi kwa miaka 20 iliyopita. Wasiliana nasi leo ili kupanga makadirio ya dari kupitia nambari ya ofisi 0703200300 ama 0706200300.

Tunauza materials za gypsum kwa bei nafuu na pia tunasafirisha hadi kwenye mjengo wako popote Kenya. Baadhi ya bidhaa tunazouza hapa Kenya ni;

 • Bodi za jipsum (Gypsum Board)
 • Chuma za bodi ya jasi
 • Plaster za bodi ya jasi
 • Mikanda za bodi ya jasi

Na nyenzo mbalimbali za mapambo ya ndani

Faida za Dari Ya Gypsum Nyumbani

 • Kupunguza joto – Kama ilivyoelezwa, dari ya jasi inaweza kusawazisha joto la ndani la nyumba. Hii inadumisha hali ya hewa ndani ya nyumba yako hata wakati wa joto kali ama baridi kali za usiku. Gypsum Board inaunda kizuizi ambacho huzuia mtiririko wa joto kati ya paa na dari. Hii inaweza kukuokoa pesa ya kutokununua kiyoyozi (kifaa cha kuleta ubaridi) kwani nyumba yako itabaki kuwa na hali wastani mwaka mzima.
 • Kuzuia Sauti – Ni muhimu kuwa na nyumba tulivu isiyovutia makelele ya nje ama makelele ya kusambaa kutoka chumba kimoja hadi kingine. Unahitaji mazingira tulivu wakati unahitaji umakini ukiwa unafanya shughuli zako na wakati wa kupumzika. Vile vile, wengi wetu hutaka kurudi kwenye nyumba tulivu baada ya siku ndefu ya kazi. Dari za plasterboard husaidia kupunguza viwango vya kelele kwa kuzuia sauti za nje kuingia ndani ya nyumba kupitia paa. Dari zetu pia huzuia sauti za kelele za ndani zisisikike nje. Utulivu wa mazingira bila kelele huongeza hisia ya usalama, faragha na faraja ya nyumba
 • Mapambo ya Ndani ya Nyumba – Dari za gypsum zinaweza kusanikishwa kitaalam na wataalam kama Gypsum Ceiling Supplies. Hubadili chumba chako kuonekana bora zaidi baada ya kupakwa rangi na kumaliziwa vizuri. Gypsum boards zinaweza kusanikishwa na kufanyiwa finishing bila kuonesha mistari ya ukutanishi wa bodi na kisha kupakwa rangi ili kutoa mwonekano mzuri.

Ukiwa unajenga au unakarabati nyumba yako, tunakushauri utumie dari za jipsam za Gypsum ceiling supplies ili kuboresha faraja yako. Bidhaa zetu zinatumia teknolojia ya Kijerumani na United Kingdom. Wasiliana nasi leo kujua kuhusu bidhaa zetu za dari na zinginezo

0
CALL US